Friday, 24 March 2017

DAH!!HUYU NDIYE MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ALIYEFANYA MAPENZI NA WALIMU WATATU




Mwanafunzi wa Shule ya Msingi nchini Tanzania kijiji cha Ruwenzera amedai kufanya ngono na walimu wake watatu kwa nyakati tofauti baada ya kuahidiwa kupewa zawadi na fedha.


Akizungumzia sakaa hilo, mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo, Masele Omary alisema kuwa Machi 7 uongozi ulikutana na kufikia uamuzi wa kumuomba mkurugenzi mtendaji wa wilaya awaondoe walimu hao baada ya kujiridhisha na maelezo yaliyotolewa na mwanafunzi huyo.

 Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo anayesoma darasa la saba, alifanya ngono na walimu hao kwa nyakati tofauti baada ya kumshawishi kumpa Sh10,000 na mwingine kuahidi kumnunulia nguo za ndani.

Alidai mwalimu Gerard Paulo alimuahidi kumnunulia nguo za ndani, huku Osner Yohana na mwingine (jina linahifadhiwa kwa kuwa hakupatikana kuzungumza) alimshawishi kwa kumpa Sh10,000 kila mmoja.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Paulo na Yohana walikana kumrubuni mwanafunzi huyo wakidai tuhuma hizo zinatokana na wao kuhoji matumizi ya fedha za ukarabati na michango ya chakula.

No comments:

Post a Comment